TAIFA STARS NA MALAWI ZATOKA SARE 0-0 JANA KATIKA UWANJA WA SOKOINE MBEYA




 http://1.bp.blogspot.com/-MV6ep7dL5Yo/T8Dxz3OWJ3I/AAAAAAACzrw/tzsLGU2uUxI/s1600/IMG_6571.jpg

FT: TAIFA STARS 0 : 0 MALAWI
Zimeongezwa dakika 4 pambano hili kumalizika.
Dakika 45` kipindi cha pili zimeshatimia na tunasubiri dakika za mwamuzi.
Dakika 40` kipindi cha pili hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Hamis Mcha `Vialli` ameingia kuchuka nafasi ya mtu
 Frank Domayo anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Kelvin Friday.
Dakika ya 33` kipindi cha pili Malawi wanafanya shambulizi hatari, lakini Dida anaokoa. 
Dakika ya 31` kipindi cha pili hakuna bao kwa timu zote.

Dakika ya 29` Malawi wanapata kona inayochongwa na Deogratius Chilambo, lakini mabeki wa Stars wanaokoa. 
Taifa stars wanafanya mabadiliko, Harun Chanongo anaingia kuchukua nafasi ya Saimon Msuva.
Taifa Stars wanafanya mabadiliko, Hamid Mao Mkami anaingia kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni.
Dakika ya 22` Malawi wanapata kona kueleka lango la Taifa stars lakini Msuva anaokoa.
Dakika ya 22` kipindi cha pili milango bado ni migumu kwa timu zote.
Dakika ya 20` kipindi cha pili, John Bocco alitandika shuti kali lakini mpira unagonga mtambaa panya.

Dakika ya 14` kipindi cha pili milango ya timu zote bado ni migumu.
Kona inachongwa kwenda lango la Taifa stars, lakini Dida anadaka mpira.
Dakika ya 4` kipindi cha pili hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Dakika ya 1` ya kipindi cha pili imetokea piga nikupige kwenye lango la Taifa stars, lakini umahiri wa Dida umesaidia.

Kipindi cha pili hapa sokoine  kimeanza

HT: TAIFA STARS 0 : 0 MALAWI
Dakika 45` kipindi cha kwanza zimeshamalizika kwa timu zote kutofungana.
Dakika ya 40` kipindi cha kwanza milango bado migumu

Dakika ya 35` kipindi cha kwanza hakuna bao. 
Taifa stars wanapata kona inayochongwa na Singano na Agrey Morris anapiga kichwa mpira huo wa kona, lakini unagonga mwamba.
Dakika ya 31` kipindi cha kwanza Malawi wanapata kona inayochongwa na John Banda, lakini Erasto Nyoni anaokoa.

John Bocco anaingiza krosi nzuri lakini kipa anaokoa
Dakika ya 24` kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake
Dakika ya 16` kipindi cha kwanza hakuna bao lolote.
Mpira umeanza hapa Sokoine.

TAIFA STARS 0 : 0  MALAWI

kikosi cha Taifa stars

1.Deogratius Munish `Dida`

2. Erasto Nyoni

3. Oscar Joshua

4. Nadir Haroub Canavaro`

5. Agrey Morris

6. Shomary Kapombe

7. Ramadhan Singano `Messi`

8. Frank Domayo

9. John Bocco

10. Amri Kiemba

11. Saimon Msuva
Previous
Next Post »