KUNA WASIWASI WACHEZAJI HAWA WA MAN U KUTOCHEZA KOMBE LA DUNIA



Phil Jones
Chris Smalling
Ashley Young
 Ashley Young  hatarini zaidi

Warning: Roy Hodgson says Manchester United players have no 'God-given right' to a place in his England squad, but Wayne Rooney is almost certainly a starter
 Wayne Rooney  ana uhakika wa kuitwa
KOCHA wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson amesema wachezaji wa Manchester United wapo hatarini kutojumuishwa katika kikosi chake kinachotarajia kwenda Brazil kushiriki kombe la dunia kuanzia juni 12 hadi juli 13 mwaka huu.
Bosi huyo wa Simba watatu ameonya kuwa wachezaji Michael Carrick, Danny Welbeck, Phil Jones, Chris Smalling, Ashley Young na Tom Cleverley wanaweza kutupwa nje ya kikosi chake kwasababu ya kiwango kibovu cha klabu yao msimu huu.
Welbeck na Carrick – kwa pamoja walifanya kazi nzuri wakati wa kampeni za kufuzu fainali za kombe la dunia, lakini kiwango kibovu cha klabu yao kitaathiri nafasi yao.
Hodgson amesema atachukua wachezaji wa kikosi chake kwa kuangalia kiwango cha klabu zao, hivyo amesema timu kama Manchester United wachezaji wake wanaweza kukosa nafasi.
“Manchester United ni moja ya klabu chache zenye wachezaji wengi timu ya taifa, lakini wachezaji lazima wakubali bahati mbaya katika soka lao la England”. Amewaambia The Independence.
“Kama klabu yao inafanya vibaya maana yake na wao hawafanyi vizuri. Kuna wachezaji wengi wanaofanya vizuri katika klabu zao, kwahiyo inawatishia nafasi yao katika kikosi cha timu ya taifa”.
 “Nina uhakika wachezaji wa Manchester United watanielewa kuwa hawana nafasi nzuri ya kucheza timu ya taifa kwa sasa, kwasababu kiwango chao sio kizuri”.
“Ni wajibu wangu kuchagua wachezaji wenye viwango bora kwa kazi tuliyonayo mbele yetu”
Wayne Rooney  hayuko fiti sana, kwahiyo nafasi yake ya kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Italia ipo kutegemeana na atakavyoimarika.
Carrick, Welbeck, Jones and Smalling  bado wana uhakika kidogo kuitwa, lakini Cleverley na Young  wapo katika hatari ya kukosa kabisa.
Hodgson atataja kikosi chake mei 12 mwaka huu baada ya kumalizika kwa ligi kuu soka nchini England.
Previous
Next Post »