Kanye West na Kim Kardashian waripotiwa kuwa wameshafunga ndoa

Baba na mama North West, Kanye West na Kim Kardashian wameripotiwa kuwa ni mke na mume rasmi waliofunga ndoa ya kiserikali.
Kwa mujibu wa Life & Style, chanzo kimesema kuwa wawili hao walifunga ndoa na kupata leseni/cheti cha ndoa wiki iliyopita huko California.
“Kim Kanye wameona tayari kwa kusaini. Walipata leseni yao California siku chache zilizopita….Kim na North wako njiani wanarudi New York City muda huu.” Kimesema chanzo hicho.
Hata hivyo muwakilishi wa Kim Kardashian alipoulizwa na NY Daily News kuhusu tetesi hizo, alikataa kuelezea.
“Bado hakuna tamko wala comment ya mwisho kuhusu ndoa yaoo.” Alisema muwakilishi wa Kim K.
Wawili hao wanatarajia kufanya sherehe ya ndoa yao jijini Parisi mwezi huu. Bado eneo la tukio halijawekwa wazi.
“Watu wanadhani itakuwa na sherehe kubwa, na nadhani itakuwa lakini…watu mia mbili lakini wote marafiki wetu wa karibu sana.” Kim Kardashian aliambia jarida la Vogue hivi karibuni.
Previous
Next Post »