TWEET BORA ZA DK MENGI KUANDIKWA KITABUNI

KITABU kitakachokuwa na mawazo yaliyoshinda kwenye shindano la tweet na Mengi kinaandikwa ili kuwapa fursa Watanzania kusoma na kuyatumia mawazo hayo bora ili kuweza kutambua fursa zilizopo zitakazowawezesha kujiajiri.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa kitabu hicho kitaandikwa baada ya shindano hilo kutimiza mwaka mmoja tangu lianzishwe Mei mwaka jana.
"Tunataka kuona mawazo hayo bora yanafanyiwa kazi, naamini yatawasaidia Watanzania wa kawaida kusonga mbele kiuchumi," alisema Dk Mengi wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo wa mwezi Machi.
Katika shindano la mwezi Machi la Tweet na Mengi, swali liliuliza toa mfano wa jinsi kitu kinavyokuwa kero kwa watu wengi, lakini kinaweza kugeuka kuwa fursa ya kibiashara.
Previous
Next Post »