Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kushoto akishangilia na Alonso kulia |
Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kulia akipiga shuti pembeni ya Dani Alves |
REAL Madrid imetwaa Kombe la Mfalme baada ya kuichapa Barcelona mabao 2-1 usiku huu Uwanja wa Mestalla mjini Valencia, Hispania.
Real walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11, mfungaji Angel di Maria akimalizia pasi ya Karim Benzema, lakini Bartra akaisawazishia Barca dakika ya 68 kwa pasi ya Xavi.
Shujaa wa Real hii leo alikuwa na nyota wa Wales, Gareth Bale aliyefunga bao la ushindi dakika ya 85 kwa pasi ya Fabio Coentrao.Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alikuwa nje leo akiendelea kuugulia maumivu yake na aliungana na wenzake kuwapongeza baada ya mechi kwa ushindi huo.
Baada ya kunyakua taji la kwanza msimu huu, Real sasa inaelekeza nguvu zake katika mataji mengine mawili, La Liga na Ligi ya Mabingwa ambako imefika hatua ya Nusu Fainali na itamenyana na mabingwa watetezi, Bayern Munich.
Kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, Real inachuana na Atletico Madrid walio kileleni na Barca walio nafasi ya tatu.
Angel di Maria akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Real
Bartra akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Barcelona
Gareth Bale akipiga shuti mbele ya Javier Mascherano
EmoticonEmoticon