TAZAMA VIDEO NA PICHA MTO RUVU WAFURIKA, MAGARI YAKWAMA



Mto Ruvu unavyoonekana kwa mbali, maji yamejaa kiasi cha daraja kushindwa kuonekana















Mvua zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo zimezidi kuleta maafa nchini, mabasi ya abiria na magari ya mizigo yanayoenda mikoani na kutoka mikoani yamekwama kuendelea na safari zake baada mto Ruvu kufurika.

Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema Polisi wamezuia magari kuvuka katika daraja la Mto Ruvu kwani hakuna uhakika kama lipo au tayari limeshavunjika mapaka hapo maji yatakapopungua na hakuna dalili ya maji hayo kupungua kwa sasa.

Askari hao wamelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya makaravati yaliyokuwa jirani na mto huo kusombwa na maji hivyo wana wasiwasi inawezekana kuwa hata daraja hilo linaweza kuwa limeondoka.


Previous
Next Post »