Mtu
mmoja amepoteza maisha papo hapo baada ya gari alilokua akitembelea
Corola Primio lenye nambanza usajili T 444 CST kuangukiwa na Lori aina
ya Scania T 424AEB lililo beba Kontena na kuvutwa na tela lenye namba za
usajili T 653ABW ambalo lilipinduka hii leo mchana katika eneo la
Temeke Vetenary jirani na soko barabara kuu ya Mandela, Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam. Mtu mmoja mwanamke alinusurika katika ajali hiyo
baada ya kutoka salama na kutoweka.
Wananchi
wakiwa wamekusanyika wakiangalia uokoaji kutoka kwa kikosibcha zimamoto
cha jiji la Dar es Salaam wakisaidiana na wananchi.
Gari hilo dogo likiwa limeharibika vibaya likisogezwa tayari kwa kukatwa na kutoa mwili wa marehemu.
Lori hilo likiwa limeanguka na kulaloa gari hilo dogo lililokua likitokea eneo la Tazara sambamba na lori hilo.
EmoticonEmoticon