Website Ya Man Utd Imeweka Wazi Jibu La Van Persie Kuhusu Kuhama Utd.


pp

Kutoka kwenye mtandao wa Man Utd ‘manutd.com’ mshambuliaji wa klabu hiyo Robin van Persie amesema anataka kubaki Man Utd na atatia wino mkataba mpya baada ya mkataba wake wa sasa kuisha mwaka 2016 ili kuendelea kubaki Manchester United.

Dutchman hiyo anasema ilibidi ajibu tuhuma hizo za kuhama Old Trafford zinazo sambazwa na vyombo vya habari Uingereza.
Van alisema “Kwa sasa sijali wanaoponda mchezo wangu uwanjani na mapungufu yangu sababu baadhi ya maneno yao ni kweli, Sipendi watu kuniongelea kama sina kichwa changu na maamuzi yangu, mimi ndio najua najiskiaje na nataka nini, Nina raha nikiwa Man Untd ndio maana nikatia wino mkataba wa miaka minne na nita saini mkataba mpya baada ya miaka miwili ”
Robin pia amesema ana mahusiano mazuri na wachezaji wenzake na manager wa Man Untd David Moyes.
Previous
Next Post »