Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM).Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi.
Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM).Kushoto ni Afisa Ustawi Mwandamizi Mkuu kutoka kutoka Wizara hiyo, Josephine Lyengi na Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.(Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO).
Na Frank Mvungi
WIZARA ya Afya na Ustawi wa jamii imefanikiwa kuajiri watumishi 27,795 katika kipindi cha mwaka 2005/2013.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Nsachris wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam wakati akizungumzia mafanilkio ya mpango wa maendeleo ya Afya ya msingi (MMAM)
Mwamaja amebainisha kuwa lengo kuu la mpango huo ni kusogeza huduma za afya ya msingi kwa wananchi wote kwa ubora unaokubalika karibu zaidi na wanakoishi.
Alisema aidha malengo mahususi ya mpango wa MMAM ni kuongeza, kurekebisha, kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya na ustawi wa jamii na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa usawa na kuwafikia wananchi wote.
Aliongeza kuwa mpango huo unalenga kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu, vifaa tiba na dawa zenye ubora katika vituo vya afya ili kuhakikisha utendaji ulio bora.
Mwamwaja aliongeza kuwa ni vyema wananchi wakashiriki katika kuhakikisha kuwa mfumo huo unafanya kazi ili kuleta tija na kufikiwa kwa malengo ya mpango huo.
Katika mpango huo wa MMAM, Serikali imeongeza udahili kwa wanafunzi wa wanaosoma kada za Afya nchini kwa mwaka 2012/2013 hadi kufikia 7,956.
Mwamaja aliongeza kuwa Wizara ya Afya imepewa kibali cha kuwapangia vituo vya kazi watumishi 11,221 wa kada za afya ambapo zoezi hilo linaendelea.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia miongozo ya Kitaifa na Kimataifa ikiwemo Dira ya Taifa 2015, MKUKUTA II, malengo ya millennia,Ilani ya uchaguzi na sera ya Taifa ya Afya.
EmoticonEmoticon