·
MWANAMUME MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UKWAVILA
AUAWA KATIKA UGOMVI.
· MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUGOGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
· MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA CHOO.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MWANAMUME MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA MOJA LA MPOSOLE (35) MKAZI WA
MUHONGOLE ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MAKALI SEHEMU ZA
KICHWANI NA SHINGONI NA MTUHUMIWA AITWAYE
VENANCE MUYINGA UMRI KATI YA MIAKA 30-35, MKAZI WA UKWAVILA. TUKIO
HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA 00:01HRS
USIKU WA KUAMKIA TAREHE 08.03.2014 HUKO KATIKA KIJIJI CHA UKWAVILA, KATA YA
MUHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI
ULIOTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA TANGU
MWAKA 2013. MTUHUMIWA ALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO WAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KATIKA VYOMBO HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGOGWA NA GARI
WILAYANI RUNGWE.
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI
MPUMBULI DARASA LA TANO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THOMAS PHILIPO (13) MKAZI WA MPUMBULI AMEFARIKI DUNIA WAKATI
AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MAKANDANA - TUKUYU BAADA YA
KUGOGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE. TUKIO
HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 08.03.2014
MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MPUMBULI, KATA YA MPUGUSO,
TARAFA YA PAKATI, BARABARA YA TUKUYU/KYELA WILAYA YA RUNGWE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA
AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI HIYO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
PIA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI WATUMIAPO
BARABARA IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA
NI PAMOJA NA KUVUKA KATIKA ALAMA ZA KUVUKIA [ZEBRA CROSSING]. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA
KATIKA CHOO.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU (03) ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA INNOCENT OSCAR MKAZI WA KIJIJI CHA
ILUNDO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO LA CHOO KILICHOKUWA
KIMEJAA MAJI. TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
08.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS
ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILUNDO, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE,
WILAYA YA RUNGWE. CHANZO CHA KIFO CHA
MTOTO HUYO NI BAADA YA KWENDA KUJISAIDIA KATIKA CHOO HICHO AKIWA PEKE YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI
KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA WITO KWA WAMILIKI WA NYUMBA
KUWA NA KAWAIDA YA KUANGALIA UIMARA WA VYOO HASA VYA SHIMO ILI KUEPUKA MADHARA
YANAYOWEZA KUTOKEA KAMA HAYO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUKIA MASHIMO
AMBAYO HAYATUMIKI NA KUFUNIKA VISIMA VILIVYOPO KATIKA MAENEO YAO KWANI NI
HATARI KWA WATOTO UKIZINGATIA TUNAELEKEA KATIKA KIPINDI CHA MVUA NYINGI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO].
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BESTA HASSAN (48) MKAZI
WA KYIMO AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20 KATIKA NDOO YA
PLASTIC. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 08.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI
NA KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA
MTENGENEZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon