Baada kufanya kazi kwa miaka 12 akiwa chini la Interscope Records, Aftermath Entertainment na Shady Records, kiongozi wa G-Unit 50 Cent ametangaza kujitoa kiroho safi na kutangaza kampuni mpya itakayohusika na usambazaji wa kazi zake.
Kwa mujibu wa Sacramento Bee, 50 Cent ameutangaza uamuzi huo jana (February 20) ambapo ameeleza kuwa yeye na G-Unit wamesaini mkataba mpya na kampuni ya usambazi wa kazi zake dunia nzima ya Caroline/Capito/UMG.
50 Cent amewashukuru Dr. Dre na Eminem katika tamko lake hilo ambao wanahusika na Aftermath Entertainment na Shady Records, na kueleza kuwa amekuwa na mafanikio makubwa sasa kwa kuwa walimpa nafasi.
“I have great success to date with Shady/Aftermath/Interscope and I’d like to thank Eminem and Dr. Dre for ginving me an incredible opportunity. I’leaned so much from them through the years. I am excited to enter this new era where I can Carry out my creativity vision.” Alieleza 50 Cent.
Kufuatia uamuzi huo wa 50 Cent, rapper Eminem ameyatoa ya moyoni huku akielezea urafiki kati yake na 50 Cent.
“Mimi binafsi na Shady Records tunajivunia nafasi ya kuchangia katika sehemu ya kazi ya 50. Shady isingeweza kuwa ilivyo bila 50 Cent.
“Nimeendeleza urafiki mkubwa na 50 kwa miaka mingi, na hiyo haitabadilika. Tunafahamu 50 atakuwa na mafanikio katika hali yake mpya, na tunabaki kuwa supporters wake yeye na G-Unit.” Amesema Eminem.
Katika kipindi cha miaka 12, 50 amefanya miradi mingi na Shady/Aftermath/Interscope ikiwa ni pamoja albam ya Get Rich or Die Tryin’, The Massacre, Curtis na Before I self Destruct na zote zitaendelea kuuzwa na Shady/Aftermath/Interscope.
EmoticonEmoticon