Nidhamu mbovu ya matumizi Serikalini imeendelea kuitesa Serikali baada ya wabunge kuwataka mawaziri kuwajibika na kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria watendaji wake wanaojihusisha na ubadhirifu na wizi wa fedha za Umma.
Wakichangia kwa nyakati tofauti taarifa za kamati za Bunge za Hesabu za Serikali na Serikali za Mitaa na ile ya Bajeti baadhi ya wabunge wamependekeza kufilisiwa kwa watendaji wanaofuja fedha za Umma ili kufidia hasara huku wengine wakiwatetea mawaziri na kubainisha kuwa kuwawajibisha siyo suluhisho.
Wabunge hao akiwemo Mbunge wa Singida Magharibi MOHAMED MISSANGA, Mbunge wa Nkasi Kusini DESDERIUS MIPATA na mbunge wa Viti Maalum MUHONGA RUHWANYA wamesema katika mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa usimamizi wa fedha ni muhimu na kuishauri Serikali ipunguze utegemezi kwa wahisani.
EmoticonEmoticon