WILAYA YA MBARALI – AJALI YA MAGARI
MAWILI KUGONGANA NA
KUSABABISHA
VIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 24.12.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO ENEO LA MASHAKA KATA YA IGURUSI TARAFA YA ILONGO
WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI NO. T.843 CKL/T693 CKL AINA NA SCANIA
LIKIENDESHWA NA MUGONI S/O LUSENGA,
MIAKA 32, MSUKUMA, MKAZI WA DSM ALIGONGANA USO KWA USO NA GARI NO. T830.BQJ AINA YA T/SALOON LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GODFREY S/O BONIFAS, MGANGA MTAFITI
MKAZI WA DSM NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU AMBAO BADO
HAWAFAHAMIKA MAJINA YAO WALA ANUANI KATI
YAO WANAWAKE WAWILI NA MWANAUME MMOJA WALIOKUWA KATIKA GARI NO. T.830 BQJ T/SALOON NA DEREVA WA GARI
HILO AMEJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA
CHIMALA MISSION. CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI WA GARI NO. T.830 BQJ KUTAKA KUYAPITA MAGARI
YALIYOKO MBELE YAKE. DEREVA WA GARI NO. T.843
CKL/T.693 CKL AINA NA SCANIA
AMEKAMATWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI HASA KIPINDI
HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUEPUKA MWENDO
KASI KWANI UNAUA NA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA.
WILAYA YA MBEYA MJINI –
KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 24.12.2013 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO AIRPORT, KATA YA IYUNGA,
TARAFA YA IYELA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA BONIFACE S/O SAJILE,
MIAKA 24, DEREVA NA MKAZI WA IGURUSI AKIWA NA BHANGI KETE NNE SAWA NA UZITO WA GRAM
20. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MARA BAADA YA KUPEKULIWA KWENYE MIFUKO YAKE YA
SURUALI. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA
ANATOA WITO KWA WAKULIMA KUACHA KULIMA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
BADALA YAKE WAJIKITE KATIKA KULIMA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA.
[B.N.MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon