Na:
Meshack Maganga- Iringa.
Ndugu zangu, tunapoelekea kuaga
mwaka huu wa 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, nimepata muda wa kukaa na
kumshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea, ninamshukuru Mungu pia kwa kupata
marafiki wapya kupitia mitandao ya kijamii na pia kupitia mtandao huu, Kuna
walio nipigia simu na kuniandika barua pepe na kuna walionitembelea nyumbani
Iringa kujifunza Kilimo cha Mboga na kile cha miti. Ninawashukuru sana wote.
Karibuni tena na ninawatakia mafanikio mema kwa mwaka ujao.
Mwaka
ujao wa 2014 Usikubali watu wenye mtazamo hasi, watu wanao haribu majina ya
wenzao, wenye viburi, watu wasiokuwa na shukrani kwa wenzao ama kwa serkali,
ama ajira inayo kupotezea muda bila kutimiza malengo yako iendelee kukupotezea
muda wako na kukuumiza kisaikolojia na kurudisha nyuma ndoto yako... Jilinde,Jipende. “Don't die a copy”
Mwaka huu ujao, Jitengeneze kiasi
ambacho utapendwa na kuzungukwa na watu watakaokusaidia kuyafikia uyatakayo (Malengo
yako ama ndoto ya maisha yako) na
wafanye wafurahi kuwa na wewe. Wanaweza kuwa wateja wako,marafiki zako,waajiri
wako,wafanyakazi wako,wasaidizi wako,nduguzako, wajasiriamali wenzako.
wafanyabiashara wenzako mahali popote ulipo.Fanya mambo ambayo yatawafanya
wajue kuwa bila wewe yasingetokea. Uwezekano huo upo kwasababu wapo wengine
wanafanya hivyo na tunawaona na kuwasikia. Mwimbaji mmoja wa nyimbo za njili wa
hapa Tanzania ameimba kwa kusema ‘ katika yale yale yanayowatoa roho watu ndiyo
hayohayo wengine wanafanikiwa’
Hakikisha kuwa unatumia muda wako
vizuri. Ishi maisha kwa manufaa usipoteze muda duniani.Muda ndio maisha yako ya
kuishi duniani, wengine wanaendelea amka na wewe ufanye kitu.
Jifunze na fanya mambo mapya kila
siku ambayo hujawahi fanya hata kama ni mapya duniano.Kumbuka kuwa dunia hii
itabaki kuwa na mapungufu siku zote kama hutafanya cha kwako cha kipekee
ulichonacho. Jisukume kwenda mbele na kuwa huru kuishi kimanufaa. Na jifunze
kutafuta uwezekano katika kila kitu kwani kila kitu kinawezekana kwa
atakayetafuta njia ya uwezekano.Fursa zipo Tanzania na hakuna nchi yenye fursa
za kufanikiwa kama Tanzania amua kufumbua macho uzione, zipo hata ukibisha
zipo. Moyo wako, akili yako na mwili wako vikubali na kupenda kitu hicho
hutachoka kufanya Na lazima utasababisha kitu.
Na kwa kipindi cha mwaka huu ujao, acha
kuwanyooshea vidole wengine wewe fanya kwa nafasi yako na kwa muda wako kwa
kuwa msaada kwa wengine. KUMBUKA Tanzania inarudishwa nyuma na watanzania
wanaowanyooshea wengine vidole wakati wao hawajafanya kitu chochote. Kuwa ‘role
model’ na ‘mentor’ wa watu. Jitolee ikibidi.
Ukifanya hayo lazima dunia itageukia
upande wako.Na ukumbuke kuwa ipo nafasi duniani kwa binadamu atakayeamua
kujitengenezea nafasi yake. Kumbuka kuwa Tanzania haiwezi kutambulika bila
wewe,haiwezi kuheshimika bila wewe na heshima ya Tanzania inaanza na wewe
kimafanikio,kitabia,kiutamaduni,kielimu,kibiashara na kimtazamo.
Jifunze kusema kuwa Tanzania ni yako na bila wewe Tanzania haiwezi
kuitwa Tanzania.
Ninawatakiwa mafanikio mema kwa kwa
mwaka huu ujao wa 2014, tufanye kazi, tuanzishe miradi, tununue mashamba ama
viwanja, tuwe wapya, tuache lawama, AMUA KUFANIKIWA 2014.
meshackmaganga@gmail.com
0713 48 66 36/ 0767 48 66 36.
EmoticonEmoticon