BAADHI YA VITUO VYA TV KENYA VYAFUNGA MATANGAZO YAO UNATAKA KUJUA KWANINI SOMA HAPA
Mashirika makuu ya Nation Media , Standard na Royal media service yaliwasilisha maombi mbele ya mahakama kutaka kupewa muda zaidi kabla ya kubadilisha mfumo wa digitali ambao ulibidi kuanza Jumatatu huko Kenya.
Kutokana na hatua hiyo mamilioni ya watazamaji na mashabiki wa vituo vya NTV, KTN citizen QTV na vituo vingine hawakuweza kuona matangazo yao na vipindi wanavyopenda.
Baada ya kushindwa mawakili wa vituo hivyo vitatu walisema hawana budi bali kuheshimu sheria lakini wamesema wanafikisha malalamiko yao mbele ya mahakama ya ruifaa Jumanne katika lengo la kubadili uwamuzi wa jaji Majanja.
Jaji huyo alikataa pia pendekezo la mashirika hayo ya televisheni kupewa muda wa siku 30 kuzima matangazo yao ya analogue na kubadilisha katika digitali.
Kufuatana na tume ya mawasiliano ya kenya CCK utaratibu ulibidi kuanza tarehe 13 disemba lakini mahakama ilichelewesha kwa siku 10 ili kusubiri uwamuzi wa jaji hiyo Jumatatu.
EmoticonEmoticon