“PRESS RELEASE”
TAREHE 07. 08. 2013.
WILAYA YA MBARALI
- MAUAJI
MNAMO TAREHE 05.08.2013 MAJIARA YA SAA
22:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ULAMBULE
WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. JUMA S/O ADAM ,MIAKA 22,
MSANGU,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA
ULAMBULE ALIUAWA KWA KUKATWA
MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE
NA KUNDI LA WATU WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUKUTWA
AKIIBA MPUNGA SHAMBANI KWA
EMANUEL S/O ERASTO,MIAKA 24,MSANGU,MKULIMA MKAZI WA ULAMBULE AMBAYE
AMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA DHIDI YAO
ZIWEZE KUCHUKULIWA MARA MOJA.
WILAYA
YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 06.08.2013 MAJIRA YA SAA 14:00 HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
MAWENI KIJIJI CHA MKWAJUNI WILAYA YA
CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WALIMKAMATA
MARIA D/O PASKALI, MIAKA 49,MLUNGWA,MKULIMA MKAZI WA MAWENI AKIWA NA BHANGI
YENYE UZITO WA KILOGRAM 10. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO NDANI YA NDOO. MTUHUMIWA NI MKULIMA NA MUUZAJI WA
BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
WILAYA
YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 06.08.2013 MAJIRA YA SAA 07:00 HRS HUKO KATIKA ENEO LA MWANJELWA
JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA HASHIMU S/O LWILA, MIAKA 26,MKINGA,MKULIMA MKAZI WA
MAWENI AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 190 YENYE UZITO WA GRAM 950. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI WA BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 06.08.2013 MAJIRA YA SAA 14:00 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
UHABILA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIWAKAMATA 1.JULIUS S/O
NYAGAWA,MIAKA 47,MSANGU,MKULIMA NA 2.
ESTHER D/O NYAGAWA,MIAKA 59,MKULIMA,MSANGU WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA UHABILA
WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO]
UJAZO WA LITA 4 NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO. WATUHUMIWA NI WAUZAJI
WA POMBE YA MOSHI [GONGO] TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE
HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon