50 Cent Aponea chupu chupu Kwenda Jela Miaka 5 Na Kulipa Milioni 81 Za Faini, Fahamu Zaidi Hapa


Kufuatia mashtaka dhidi ya rapa 50 Cent kumshambulia kumpiga pamoja na kuharibu mali za Mama wa mtoto wake, mwishoni mwa mwezo Juni, msanii hatimaye amesimamishwa mbele ya jaji na kupatikana hana hatia katika kesi hii iliyochafua kwa kiasi kikubwa jina lake.



Sambamba na maamuzi haya ya Jaji, msanii huyu pia amepewa amri ya kukaa mbali na Mama Watoto wake huyu ambaye anafahamika kwa jina Daphne Joy, na pia ametakiwa kusalimisha silaha zake zote za moto anazomiliki.

50 Cent na Baby Mama Daphne Joy

Hatua hii ni kutokana na rekodi za rapa huyu katika kuvunja sheria, na katika kesi hii, endapo angepatikana na hatia, angetakiwa kulipa faini isiyopungua dola 50,000 ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 81 za Tanzania, pamoja na kifungo cha miaka isiyopungua mitano jela.

Previous
Next Post »