Unene Kupita Kiasi Pamoja Na Kuonewa Sana Utotoni Ndicho Kitu Kilichompatia Star Huyu Wa Kenya Akili


 
 
Mwanamuziki mkongwe wa kike kutoka nchini Kenya, Amani ambaye kwa sasa anatamba na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina Kiboko Changu, amefafanua kuwa, katika kipindi alichokuwa kimya kimuziki, amekuwa akijishughulisha zaidi na shughuli za hisani, ikiwepo kuzungumza na vijana kuwashauri na kuwapa mawazo chanya juu ya maisha hasa kutokana na historia yake na uzoefu wa utotoni.
Msanii huyu ameweka wazi kuwa amekuwa akifanya kazi hii hasa kutokana na historia yake alipokuwa madogo, ambapo ameweka wazi kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa hajikubali kutokana na kuwa mnene kupita kiasi na kuonewa na wengine, kitu kilichokuwa kinammaliza kisaikolojia.

Msanii huyu ameseme kuwa, fani ya kuimba ndiyo iliyomsaidia kusimama na kujiona kuwa yeye ni muhimu na ana nafasi katika jamii, kitu ambacho kimemsaidia kufika hapa alipo, na ndiyo sababu ya yeye kutumia muda wake kusaidia wengine.
Previous
Next Post »