Dar es Salaam. Wakati mvutano kati ya Serikali na wadau
mbalimbali kuhusu pendekezo la kufutwa kwa tozo ya kodi ya laini za simu
‘Simcard tax’ ya Sh1,000 ukiwa haujapoa, Chama cha Wenye Mabenki nchini
(TBA) kimeibuka na kuitupia lawama Serikali kwa kuanzisha kinyemela
sheria ya kodi ya kuhamisha fedha kutoka benki.
Taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na
Mwenyekiti wa TBA, Dk Charles Kimei imesema kuwa Serikali kupitia Sheria
ya Fedha ya mwaka 2013 (The Financial Act 2013) ilitangaza ongezeko la
tozo hiyo ya kodi kwa asilimia 0.15.
Kutokana na tozo hizo, gharama za kibenki kwa
wateja zitaongezeka na kumlazimisha mteja aliyekuwa anatuma Sh 10
milioni kwa njia ya Mfumo wa Malipo Makubwa na ya Haraka (TISS) kwa
gharama ya Sh10,000, sasa atalazimika kutumia Sh25,000 kutuma kiwango
hicho cha fedha.
Alipoulizwa kwa njia ya simu jana jioni kuhusu
tozo hizo Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa aliomba atafutwe baadaye
kwa maelezo kuwa yupo katika kikao.
Hata hivyo, alipotafutwa tena simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu.
Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imethibitisha kupitishwa kwa sheria hiyo, huku Mkurugenzi wa Huduma na
Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo akilieleza gazeti
hili jana kuwa walitoa barua kwa TBA tangu Julai 16, kuwataka kuanza
utekelezaji wa sheria hiyo.
Sheria hiyo inasema; Kutakuwa na tozo ya kodi kwa
fedha zinazohamishwa kupitia benki, taasisi ya fedha au kampuni ya simu
kwa tozo ya asilimia 0.15 kwa kiwango cha fedha kinachozidi shilingi
30,000… Tozo hiyo haitahusu uhamishaji wa fedha kutoka benki moja kwenda
nyingine, taasisi za fedha, Serikali na shughuli za kibalozi.”
TBA inasema, Serikali imeingiza tozo hiyo
kinyemela kwenye sheria na kwamba haikuwemo kwenye hotuba ya bajeti ya
Wizara ya Fedha mwaka 2013/2014 wala kwenye mapendekezo ya muswada wa
sheria ya fedha, kwamba ilitolewa kama mabadiliko kwenye sheria.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa iwapo tozo
iliyopendekezwa itatumika kama ilivyo, kutakuwa madhara makubwa katika
mzunguko wa fedha kwa kuwa asilimia 12 pekee ya watu wote nchini, ndiyo
wanaotumia huduma ya benki.
Shirikisho hilo lilifafanua kuwa mabenki yanatumia
mfumo wa kuhamisha fedha kwa njia ya simu ili kupunguza pengo lililopo
baina ya watu wanaotumia benki na wasiotumia huduma hiyo.
“Tozo hilo itaongeza ufisadi na changamoto
nyingine za kiuendeshaji kwa kuwa zitawapa watu nafasi ya kutafuta njia
ya kukwepa kodi hiyo mpya” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Shirikisho hilo limebainisha kuwa limeshaiandikia
barua TRA na Waziri wa Fedha, kuwataka wakutane kuzungumzia suala hilo
na kwamba iwapo Serikali haitaondoa tozo hiyo wananchi wajiandae kulipa
kodi hiyo mpya.

Source :MWANANCHI
EmoticonEmoticon