Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema wizara haina mpango wowote kwa sasa
kuhusiana na wanafunzi waliofeli kidato cha nne mpaka pale Tume itakapomaliza
kufanya kazi yake ndipo itaamua nini cha kufanya. Mulugo aliliambia NIPASHE
kuwa wizara inasubiri Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imalize
kufanya kazi yake, ndipo itatoa uamuzi nini kifanyike juu ya wanafunzi
hao.
“Kwa sasa siwezi nikasema
chochote kwani tume imeundwa ili kulifanyia kazi jambo hilo, hivyo tunasubiri
wamalize kufanya kazi yao ndipo tutatoa kauli ya nini kifanye juu ya wanafunzi
walio feli kama ni kurudia tena mtihani au la,” alisema Mulugo.
Alitoa ufafanuzi huo baada
ya kuulizwa wizara yake inazungumziaje juu ya mpango wa Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuandaa mafunzo ya kozi ya
muda mfupi kwa vijana wote waliofeli mkoani humo ili kuwapima kama wapo
wanaaoweza kusaidiwa kuendelea na elimu ya cheti.
Msambatavangu alitoa uamuzi
huo baada ya makubaliano yake na baadhi ya vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha
Tumaini (IUCO) na Chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) na kukubaliana kutoa mafunzo hayo
yatakayo anza Machi mwaka huu.
Mulogo alisema kuwa ni wazo
lenye mpango mzuri wa kuwasaidia vijana wengi ambao ni kama wamekumbwa na tatizo
kwa sasa, hivyo anacho kifanya Mwenyekiti huyo hakina madhara yoyote na
anafanya kama raia mwema aliyeguswa na matokeo hayo
CHANZO:
NIPASHE
EmoticonEmoticon