Mrembo
chipukizi amekutwa amekufa kwa kuchomwa kwa visu huku binti yake wa
miaka mitatu 'akilia pembeni yake kwenye dimbwi la damu', wamesema
marafiki jana.
Mwili wa Linah Keza, mwenye miaka 29, ambaye inafahamika alishiriki
kwenye Shindano la Miss Africa 2010, ulikutwa kwenye ghorofa moja huko
King Edward Road, Leyton, juzi mapema asubuhi.
Tukio hilo liliripotiwa kwenye Tume Huru ya Polisi ya Malalamiko, ambayo
itatazama mawasiliano yake waliyokuwanayo polisi na mwanaume mwenye
miaka 38 ambaye amekamatwa kuhusiana na kifo chake.
Madaktari wa Huduma za Gari la Wagonjwa London waliongozana na polisi
kwenda mahali hapo kabla ya Saa 10:30 alfajiri, lakini Linah, raia wa
Rwanda anayeishi London, alikuwa ameshatangazwa kufariki eneo la tukio.
Inafahamika kwamba binti yake alikuwa mahali hapo wakati wa shambulio hilo, kwa mujibu wa fafiki mmoja wa familia hiyo.
Herbert Muhire alisema: "Binti (yake) amepelekwa kwenye uangalizi na
kupatiwa tiba ya kisaikolojia na matukio mengine baada ya kukutwa akilia
kando ya mama yake huyo aliyekuwa amelala kwenye dimbwi la damu.
"Familia na marafiki wameelezewa jinsi alivyokuwa ameuawa na kufa kifo cha kutisha.
Rambirambi kwa Linah kutoka kwa marafiki na jamaa ziliachwa kwenye ukurasa wa Facebook uliofunguliwa mara baada ya kifo chake.
Azun Jezan aliandika: "Huzuni mno, roho yake ilale mahali pema peponi na
binti yake na familia wajazwe nguvu katika wakati huu mgumu wa huzuni."
Mwingine, Justine Twongyeirwe, aliandika: "Nitakumbuka tabasamu lako mpenzi Linah. Ulale Mahali Pema."
Jana asubuhi, ukurasa huo ulikuwa na wafuasi zaidi ya 500 na baadhi
walituma picha za Linah, ambaye alifanya kazi kama mrembo na kusomea
huduma za jamii kwenye Chuo Kikuu cha Wolverhampton.
Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo mwenye miaka 38 alikamatwa baada ya
kujisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi cha north London juzi.
Msemaji wa polisi alisema: "Uchunguzi wa mauaji umeanza baada ya mwanamke huyo kushambuliwa huko Leyton.
"Polisi waliitwa na Huduma za Gari la Wagonjwa London majira ya Saa 10:29 alfajiri ya Jumatano kwa ripoti za kuchomwa kwa visu.
"Maofisa na Huduma za Gari la Wagonjwa walifika na mwanamke huyo mwenye
miaka 29 alikuwa ametangazwa kufariki kwenye eneo la tukio."
Uchunguzi wa mwili wake ulipangwa kufanyika majira ya Saa 5 jana asubuhi kwenye Mochari ya Walthamstow.
EmoticonEmoticon