Mwanamke mmoja na mwanae wamefanya kitu ambacho si rahisi kufanyika. Na sasa wameingia kwenye kwenye mahusiano... mazito ya kimapenzi kati yao na wanataka kuonana. Mama huyo aitwe Betty Mbereko hivi sasa ana ujauzito wa miezi sita na anategemea kupata mtoto na huyo mwanae.
“Hebu fikiri, kwa jitihada zangu binafsi nimeweza kumpeleka shule mwanangu bila ya msaada wa mtu yoyote. Ila sasa mnamuona mwanangu anafanya kazi mnaanza kunituhumu kwamba nimefanya kitendo kibaya. Acheni na mimi nifaidi matunda ya jitihada zangu” mwanamke huyo alisema.
Mbereko (40), toka Mwenezi Masvingo nchini Zimbabwe ambaye ni mjane wa miaka 12 sasa, amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtoto wake wa kwanza aitwae Farai Mbereko (23). Amethibitisha kwamba yeye ni mjamzito wa miezi sita na kwamba ameamua ni bora afunge ndoa na mwanae sababu hataki kuolewa na mdogo wa marehemu mume wake.
Wiki iliyopita Betty aliieleza mahakama ya kijiji kwamba, mahusiano yao yalianza miaka mitatu iliyopita. Aliendelea kusema baada ya kutumia hela zake nyingi kumsomesha Farai baada ya kifo cha baba yake, aliona ana haki na pesa zake na hakuna mwanamke mwengine mwenye haki na mwanae.
Farai alisema, yupo tayari kumuoa mama yake na pia yupo tayari kulipia salio la mahari ambayo baba yake alibakiza kulilipa kwa bibi na babu zake. “Najua baba yangu alikufa kabla hajamaliaza kulipa mahari ya bibi harusi na nipo tayari kuilipa,” alisema.
“Ni vyema jamii ielewe kile kinachoendelea sababu ni kweli kwamba mimi ndie niliyempa mama yangu ujauzito. La sivyo watamtuhumu yeye zaidi juu ya hili.”
Msamamizi mkuu wa shauri hilo Nathan Muputirwa alisema: “hatuwezi kuruhhusu kitu kama hiki kutokea kwenye kijiji chetu, hii ni kinyume na utamaduni wetu. Kama ni zamani wangeshauwawa wote wawili, ila kwa sasa hatuwezi kufanya hivyo sababu tunawaogopa polisi.” Aliwataka wavunje mahusiano yao ama wahame kijiji hicho haraka.
Chakufurahisha zaidi, mama na mtoto wake uamuzi walioamua kufata ni ule wa kuhama kijiji na mpaka sasa hawajulikani wapo walipohamia
2 comments
Write commentsdunia hii sijui tunakwenda wapi
Replykweli yale yaliyosemwa ndo yanatimia
ReplyEmoticonEmoticon