PICHA ZA RAIS WA SRI LANKA AKIWASILI NCHINI

Picture 2396

Ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini .

Picture 2414

 Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ikishuka  katika ndege mara baada ya kutua katika  Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam mara  baada ya kuwasili nchini .

Picture 2427

 

Rais wa  Jakaya Kikwete akizungumza na mgeni wake Rais  wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa mara baada ya kumpokea katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini .

Picture 2447

Rais  Jakaya Kikwete akiimba wimbo wa taifa akiwa na  mgeni wake Rais  wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa mara baada ya kumpokea katika  Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere ilioko jijini Dar es Salaam mara  baada ya kuwasili nchini .

Picture 2455

 Gwaride  maalum likitoa heshima  kwa Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa katika  Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam.

Picture 2502

 Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa na  Rais   Jakaya   Kikwete wakiangalia kikundi cha ngoma katika  Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam.

Picture 2471

 Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa akitoka kukagua gwaride maalum katika  Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam mara  baada ya kuwasili nchini .(Picha zote na Magreth Kinabo – maelezo).

 

Lorietha Laurence –Maelezo

Rais  wa  Sri  Lanka  Mahinda Rajapaksa amewasili leo nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Jakaya  Kikwete katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius K.Nyerere jijini Dares Salaam.

Rais huyo aliwasili nchini majira ya saa 3:55 akiwa amebebwa na Ndege aina ya Air bus 340 akiwa na wasaidizi wake.

Aidha   Rais huyo alipata nafasi ya kukagua gwaride  maalum lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi hayo  na kufuatiwa na  wimbo wa Taifa wa Sri Lanka  na Tanzania , pia  alipigiwa   mizinga 21 ikiwa ni  heshima ya kumkaribisha  nchini .

Rais  huyo  alipata nafasi ya kutumbuizwa na vikundi vya Ngoma za Utamaduni vilivyokuwepo  uwanjani hapo  na kuelekea katika gari maalum liloandaliwa kwa ajili yake na kuelekea  katika Hoteli ya Serena.

Baadaye  Rais  huyo atembelea  Ikulu  jijini  Dar es Salaam mnamo  saa 11:00 jioni  kwa ajili ya  kutia saini  mikataba  ya  kiuchumi  baina  ya Tanzania na Sri lanka kwa lengo la  kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi.  Pia  atafanya mazungumzo rasmi na Rais Kikwete na kushiriki dhifa ya kitaifa.

Rais huyo atakuwepo nchini kwa muda wa siku tatu,ambapo Juni 28,  mwaka huu  atatembelea  Hekalu la Kibudha lililopo Upanga,jijini Dar se Salaam lililojengwa na Sri Lanka miaka 93 iliyopita.

Aidha  Rais  Rajapaksa anatarajiwa kushiriki katika Jukwaa la Ushirikiano  kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue)utakaofanyika kuanzia Juni  28  hadi Julai Mosi, mwaka huu.

Rais  huyo  anatarajiwa kuondoka nchini  Juni 29, mwaka huu  kurejea nchini kwake.

Previous
Next Post »