TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


 

“PRESS RELEASE” TAREHE 28. 06. 2013.



WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA       
                                                        KIFO NA MAJERUHI.










MNAMO TAREHE 27/06/2013 MAJIRA YA SAA 07:30HRS  HUKO KATIKA KIJIJI CHA  MAJIMAZURI BARABARA YA MBEYA/CHUNYA  WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA MKOA WA MBEYA .  GARI N0. T. 887 AYG AINA YA SCANIA BASI LA ABIRIA  MALI YA KAMPUNI YA SABENA LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA TABORA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA  KWA JINA LA SUDI S/O HUSEIN LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO AITWAYE JOHARI D/O IMANI, MIAKA 8, KYUSA, MKAZI WA KIJIJI CHA CHALANGWA CHUNYA NA MAJERUHI 16 KATI YAO WATATU WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA  MBEYA AMBAO NI 1. DEVOTA D/O COSMAS, MIAKA 36, MJALUO, MKAZI WA MWANZA, 2. HURUMA S/O ODEN SUKULU, MIAKA 33, KYUSA, MKAZI WA ILEMI, 3. TAUSI D/O AMBONIKE, MIAKA 2, KYUSA, MKAZI WA SHINYANGA . AIDHA KATIKA TUKIO HILO MAJERUHI  AMBAO WAMETIBIWA NA KURUHUSIWA NI 1. LADSLAUS S/O ONYANGO, MIAKA 46, MJALUO, MKAZI WA MWANZA  2. NERUSIGWA S/O MWAMBAWASA, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA CHALAGWA, 3. MTOTO BOKE D/O KISIRI, MIEZI 5, MSUKUMA WA MWANZA 4. MAGRETY D/O MOSES, MIAKA 48, MSAFWA WA KYELA, 5.  RENALTH S/O MTAKYAWA RUWELENGELA, MIAKA 40, MHAYA, FUNDI MKAZI WA NYAKATO- MWANZA, 6. DOTTO D/O JOHN, MIAKA 28, MSUKUMA, MKULIMA MKAZI WA IYUNGA 7. AMBONIKE S/O SAMWELI MWANSASU, MIAKA 42, MKAZI WA MWADUI SHINYANGA, 8. JUMA S/O SALUMU KATEMBO, MIAKA 22, MNYAMWEZI, FUNDI MAGARI, 9 JENI D/O ABONIKE, MIAKA 32, MSUKUMA WA SHINYANGA, 10. STIVIN S/O WILIAM, MIAKA 40, KYUSA, MKAZI WA MWANZA 11. ADAM S/O ISSA, MKAZI WA MWANZA NA 12. MAGE D/O MBILINYI, MIAKA 13, MNGONI, MKAZI WA SONGEA  [.] CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.  MWILI WA MAREHEMU ULIFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA TARATIBU ZA MAZISHI. GARI BADO LIPO ENEO LA TUKIO. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWANYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYESABABISHA AJALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.

 

 

WILAYA YA KYELA - KUPATIKANA NA BHANGI

 

MNAMO TAREHE 27.06.2013 MAJIRA YA SAA 20:15HRS HUKO NJISI - KASUMULU WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA IMANI S/O THOMAS,MIAKA 43,MNDALI,MKULIMA MKAZI WA NJISI AKIWA NA BHANGI GRAM 200. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

 

 

Signed By,

 [BARAKAEL MASAKI - ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

 
Previous
Next Post »