Umoja
wa waigizaji wa nchini Nigeria ambao unafahamika kama Actors Guild of
Nigeria (AGN), Jumapili hii wamefanya tukio la kipekee kusherekea
mafanikio ya mwigizaji mwenzao, Omotola Jalade-Ekeinde katika tasnia
ya Burudani nchini humo.
Hatua
hii imekuja kufuatia nyota ya msanii huyu kung'ara sana kitaifa
ambapo sasa hivi amekuwa akitikisa hadi vichwa vya habari vya
kimataifa, huku ikishuhudiwa hivi karibuni akipatiwa utambuzi wa kuwa
kati ya watu 100 wenye ushawishi zaidi Duniani, kwa mujibu wa jarida
la Times.
Tukio
hili la kipekee limefanyika huko Lagos na kuhudhuriwa na wasanii
wenye majina makubwa katika tasnia ya uigizaji Nigeria.
EmoticonEmoticon