Mtuhumiwa namba mbili Joseph Ludovick wa kesi ya kula njama za kutaka kumteka na kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky aachiwa kwa dhamana

Mtuhumiwa namba mbili Joseph Ludovick (kulia) wa kesi ya kula njama za kutaka kumteka na kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky, akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam jana baada ya kuachiwa kwa dhamana. Kushoto ni rafiki yake, Hamfrey Masawe. 

 Hatimaye Ludovick Joseph Rwezaura amerejea uraiani baada ya kuachiwa huru kwa dhamana, katika kesi ya kula njama za kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.Rwezaura na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, anakabiliwa na kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Rwezaura aliachia huru jana baada ya kutimiza masharti ya dhamana na Hakimu Aloyce Katemana, baada ya kusota mahabusu takriban miezi minne tangu walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza

Previous
Next Post »