Mwisho wa wiki iliyopita
umekuwa ni wa kipekee na wa kihistoria kwa Nameless pamoja na Baby Mama
wake, Wahu Kagwi baada ya kumkaribisha mtoto mpya katika familia yao,
mtoto wa kike ambaye wamempatia jina Nyakio Mathenge.
Mtoto huyu anakuwa ni wa pili katika familia hii ya wasanii hawa
wanaokubalika sana katika tasnia ya muziki ndani na nje ya Afrika
Mashariki, akiwa ametanguliwa na Tumiso ambaye kwa sasa ana umri wa
miaka 8.
Wahu ndiye ambaye alikuwa mtu wa kwanza kuwapatia mashabiki na
wapenzi wa kazi zao za muziki ambao pia wanafuatilia kwa karibu maisha
yao habari za kuzaliwa kwa mtoto huyu, kupitia mtandao wa Facebook,
sambamba na kumtakia mume wake maadhimisho mema ya siku yake ya
kuzaliwa.
EmoticonEmoticon