Usipende
kuamka mapema, endelea kujigeuza geuza na kupiga miayo kitandani, kwani
kama hakuna papasi au viroboto, una haraka gani kuwahi kuamka?
Usipangilie
namna ya kutumia fedha zako. Upatapo fedha tu, we zitumie hapo hapo na
zikiisha wala usifikirie jinsi ulivyozitumia. Kesho itajijua yenyewe.
Usiwaze
mambo ya kuhifahi fedha benki, subiri hadi uwe na mamilioni, kwanza uta ‘save’
vipi wakati unamahitaji mengi? Hao wanaokushauri uweke fedha benki hawakuonei
huruma na mahitaji yako.
Kamwe
usijishuhulishe katika zile shuhuli nyingine ambazo unaziita za wasioenda
shule. Yani we msomi wa chuo kikuu unafanya biashara ndogo ndongo au kuwa
na mifugo au shamba? Hizo ni kwa wale wasiojua shule.
Usifikirie
kuanzisha biashara hadi malaika atoke mbinguni akuletee mtaji. Kwanza
utaweza vipi wakati huna mamilioni? Kwanza wewe hauko ‘level’ moja na hao
wanaoanzisha vibiashara vya hela ndogo. We ni wa muhimu sana.
Laumu
kila kitu, laumu serikali, laumu mabenki, kwa kutokukopesha fedha, laumu
saccos pia kwa kuwa fedha zinazowekwa huko zaweza kuibiwa au kuliwa. Laumu
bosi au mwajiri wako kwa kutokupa mshahara mkubwa wa kuweza kuwekeza.
Tumia
zaidi ya mapato yako ili kulifanikisha jambo hili, nunua zaidi vitu vya
matumizi kwa mkopo, na azima fedha kwa marafiki na ikiwezekana mkope hata mwajiri
(si utakatwa kidogo kidogo kwenye mshahara?), kama mwajiri hataki
kukukopa, basi mwombe mshahara wa awali (advance salary) ili uweze
kujinunulia unachotaka kama vile simu ya bei ghali, macheni, mapete,
mahereni ya dhahabu n.k. Maisha yenyewe mafupi inabidi ujifurahishe.
Fanya
ushindani na mavazi ya bei kubwa, hakikisha unavaa nguo zilizo katika
chati kuliko wafanyakazi wenzako au rafiki zako wote. Wakati wowote jirani
au rafiki yako anaponunua simu wewe nenda kanunue ya gharama zaidi yake
ili umkomeshe akuheshimu.
Jinunulie
gari zuri na la kifahari ambalo linagharimu mara tatu ya mshahara wako wa
mwaka mzima. Hii itakusaidia kukuweka muda mrefu ukilipa deni la gari na
sio shuhuli nyingine za maendeleo.
wape
watoto wako kila kitu wanachohitaji, kwa sababu wewe ni mzazi mzuri unayejali,
usiwaache wahangaike kupata chochote wakati wewe upo hai kwa ajili yao
mtoto hakui kwa mzazi bwana! Kwa hali hii watafanikiwa kukua wakiwa
wazembe, wavivu na hivyo kuwa masikini kiasi ambacho hawataweza kukujali
katika uzee wako. UKIFUATA HIZI KANUNI LAZIMA UTAFANIKIWA KUUKARIBISHA
UMASKINI ULIO THABITI NYUMBANI KWAKO.
EmoticonEmoticon