Azam mwenye miaka 91 ahukumiwa kifungo cha miaka 90 jela.

GULLAM JAILED

 

Mkuu wa zamani wa chama cha kiislamu nchini Bangladesh Ghulam Azam mwenye umri wa miaka 91, amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, wakati wa vita vya kupigania uhuru wa nchi hiyo mwaka 1971.

Hukumu hiyo imewakasirisha wakereketwa wa pande mbili, wapinzani wake ambao walitaka anyongwe, na wanaomuunga mkono ambao wamesema kesi dhidi yake iliendeshwa kisiasa.

Azam ambaye alikiongoza chama cha Jamaat-e-Islami wakati wa vita vya kujitenga na Pakistan, bado anachukuliwa kama kiongozi wa kiroho wa chama hicho.

Serikali ya Bangladesh imekanusha shutuma za chama hicho kuwa kesi dhidi ya Azam na wenzake ilikuwa ya kisiasa.

 Azam alikutwa na hatia katika mashtaka yote 61 yaliyokuwa yakimkabili.

Previous
Next Post »