Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Vijana Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kuhusu fikra za
kimkakati kwa Vijana jijini Dar es Salaam katika Kongamano la vijana
lililoandaliwa wa Kanisa la Nchi ya Ahadi kupitia kituo chake
kinachojulikana kwa jina la CHIMBO School of Thought.
Rai hiyo
imetolewa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel
alipokuwa akiwasilisha mada juu ya vijana kuwa na fikra za kimkakati
katika kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Vijana kinachojulika kwa
jina la Chimbo School of Thought jijini Dar es Salaam.
Profesa Ole
Gabriel amesema kuwa inakuwa ni tatizo kwa vijana kupambana na
changamoto za maisha kwa kuwa vijana wengi hawaweki mikakati katika
fikra zao.
Aidha
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa takwimu zinaonyesha takriban asilimia
35.1 ya idadi ya watu ni Vijana na ambapo vijana wanachua karibu
asilimia 70 ya nguvu kazi,hivyo wasipo kuwa na fikra na kupanga mambo
yao kimkakati nchi itapata hasara.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Chimbo School of Thought Mchungaji Harris Kapiga
amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa vijana kama nguvu kazi ya taifa
kituo chake kimenuia kubadilisha vijana wengi nchini ili wawe na
mitazamo chanya ili wajiletee maendeleo yao wenyewe.
Mchungaji
Kapiga amesema kupitia kituo chake vijana wengi wamebadilika kimtazamo
na kutoa wito kwa vijana wengi kushiriki katika makongamano mbalimbali
yanayoandaliwa kwa ajili yao ili wajifunze na kupata ufahamu wa mambo
mengi zaidi.
EmoticonEmoticon