WATU 15 WANAENDELEA KUPATA MATIBABU BAADA YA KUJERUHIWA KWENYE MASHAMBULIZI MAWILI TOFAUTI HUKO KENYA

 

Takriban watu 15 wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali mbali mbali nchini kenya, baada ya kujeruhiwa kwenye mashambulizi mawili tofauti ya Guruneti katika mitaa ya Likoni jijini Mombasa na Eastleigh katika jiji kuu la Nairobi jumapili.
Kwenye mkasa wa Likoni, watu 12 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililolenga Kanisa la Earthquake Miracle Ministries ambako mhubiri wa kanisa hilo Dominic Osano vile vile alijeruhiwa.
Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali kuu eneo la Pwani ambako baadhi yao walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Vile vile, polisi wanasema guruneti lilitupwa katika hoteli moja maarufu mtaani California eneo la Eastleigh Nairobi.
Inaarifiwa washukiwa waliokuwa ndani ya gari dogo walitoweka baada ya kurusha guruneti hiyo.
Wakuu wa polisi eneo la Mombasa na Nairobi wanasema kufika sasa hakuna washukiwa waliokamatwa kuhusiana na mashambulizi hayo mawili.
Haya yana jiri siku Nne tu baada ya Rais uhuru kenyatta na mwenzake Hassan Muhamed wa somalia kuwataka maafisa wa kiusalama kutoka nchi hizo mbili kushirikiana ili kukabili tishio la ugaidi.

Previous
Next Post »