PICHA YA MBUNGE WA MTWARA MJINI MH HASNEIN MURJI WAKATI IKIFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI

Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnein Murji (kushoto) akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara jana kusomewa shtaka la kufanya uchochezi.   

 Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnein Murji jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa akituhumiwa na kosa la uchochezi. Baada ya kusomewa shtaka hilo, mbunge huyo alirudishwa rumande kutokana na kushindwa masharti. Sharti hilo lilikuwa ni kuwa na pasi ya kusafiria, ambayo alikuwa ameiacha Dar es Salaam alikokamatwa.

 Murji amepandishwa kizimbani ikiwa ni moja ya mkakati wa vyombo vya dola kuwasaka na kuwafungulia mashtaka watu inaowatuhumu kuhusika kuchochea vurugu ambazo chanzo chake ni kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mwendesha Mashtaka ambaye ni Wakili wa Serikali, Zuberi Mkakatu aliieleza Mahakama kuwa mnamo Januari 19, mwaka huu, maeneo ya Ligula mkoani hapa mtuhumiwa alichochea watu kutenda makosa
Previous
Next Post »