TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


 


“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 06. 2013.

WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA VIFO.

 MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO VWAWA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.840 BKD AINA YA TOYOTA HARRIER LIKIENDESHWA NA DEREVA BROWN S/O MWAKIBAMBO,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O HALINGA,MIAKA 27,MKULIMA MKAZI WA ILOLO AKIWA  AMEMBEBA MTOTO WAKE AITWAE HELENA D/O SAMSON,UMRI  WA MWAKA MMOJA NA NUSU, KYUSA  NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI . TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

 
WILAYA YA KYELA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.


MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO GWAKISA ENEO LA KYELA - KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. LUKINDO S/O JOHN,MIAKA 45 NA 2. MSEMAKWELI S/O JOHN, MIAKA 27 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI RWANDA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA ZA KISHERIA  DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.

 
Signed By,

 [DIWANI ATHUMANI - ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

 
Previous
Next Post »