“PRESS RELEASE” TAREHE 18. 06. 2013.
WILAYA YA KYELA - KUBAKA
MNAMO TAREHE 17.06.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA ITUNGE WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. IPYANA S/O GIDION,MIAKA
30,KYUSA,MKULIMA / MWALIMU WA MASOMO YA ZIADA [TUITION] ITUNGE MORAVIAN MKAZI WA MTAA WA MBUGANI – KYELA ALIMBAKA MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 10, KYUSA,MWANAFUNZI DARASA
LA NNE S//MSINGI MBUGANI MKAZI WA ITUNGE “A” NA
KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI MWILINI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUWARUHUSU WANAFUNZI
ALIOKUWA AKIWAFUNDISHA KUONDOKA NA
KUBAKI NA MHANGA KISHA KUMBAKA KATIKA CHUMBA ANACHOTUMIA KUFUNDISHIA [DARASANI]
. MTUHUMIWA AMBAYE ALIWAHI KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 GEREZANI KWA KOSA LA
KUBAKA NA KUTOKA KWA RUFAA AMEKAMATWA. MHANGA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TAMAA ZA KIMWILI BADALA YAKE KUWA WAAMINIFU KATIKA MAJUKUMU AMBAYO
WAMEPEWA DHAMANA NA JAMII/TAASISI
KUYATEKELEZA KWA UADILIFU.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA.
EmoticonEmoticon