Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech kujiuzulu.

 

20136162151882734_4

 Waziri Mkuu  wa  Jamhuri  ya  Czec  Petr  Necas, ametangaza  kuwa   atajiuzulu  wadhfahuo hii leo.

Necas amekuwa akishinikizwa ajiuzulu  tangu  pale  Mnadhimu  Mkuu  wa  serikali Jana Nagyova, aliposhitakiwa  kwa rushwa  na  matumizi  mabaya ya  madaraka.

Wabunge  wawili  wa zamani akiwemo Waziri  wa  zamani  na  mkuu  wa  sasa  wa upelelezi  katika  jeshi  pamoja  na  mwenzake  wa  zamani pia  wamekamatwa. 

Rais Milos Zeman amesema  kuwa mashtaka  yao yamefunguliwa  baada  ya  polisi  kupekua  ofisi  za  serikali pamoja  na  za  binafsi  wiki  iliyopita.

Muungano  wa vyama  vinavyounda  serikali  ya  Necas  utajaribu  kuunda serikali  mpya, ambapo Kiongozi  atateuliwa  na  chama  chake  cha Civic Democratic.

Previous
Next Post »