TAZAMA DUNIA HUU INAKOELEKEA WANAWAKE HAWA WAFUNGA NDOA

NewsImages/6886818.jpg 


Wanafunzi wa wasagaji wenye asili ya Pakistan ambao wanaminika kuwa ni waumini wa dini ya kiislamu, wamefunga doa ya jinsia moja nchini Uingereza, na kuwafanya wawe wanawake wa kwanza waumini wa kwanza wa dini hiyo kuripotiwa kufunga ndo aina hiyo.

Wanawake wawili wasagaji wanaoaminika kuwa ni waislamu wamefanya sherehe ya ndoa yao ya jisia moja nchini Uingereza, wanandoa hao wasagaji wanaofahamika kwa jina la Rehana Kausar (34) na Sobia Kamar (29) walifanya sherehe ya harusi yao katika eneo la Leeds mapema mwezi huu, na baada ya ndoa hiyo waliyomba hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchini humo.

kwa mujibu wa gazeti la Independent la nchini Uingereza, limesema kuwa wanandoa hao walingia kwa mara ya kwanza nchini humo kwa ajili ya masomo katika chuo kikuu cha Birmingham.
Wanandoa hao wamekuwa wakipokea vitisho vya kuuliwa wao na familia zao zilizopo Pakistan, ambapo vitendo vya usagaji ni kinyume na sheria nchini humo.

Uingereza imetupa haki yetu ya binafsi, na uwamuzi huu ambao tumeuchukua ni uwamuzi binafsi, ambao hakuna mtu kuingilia katika maisha yetu binafsi, alisema mmoja ya wanandoa hao wakati akihojiwa na moja ya gazeti la ndani la uingereza.

Aliendelea mwanandoa huyo kwa kusema tatizo la Pakistan kwamba kila mtu anadhani kwamba anajukumu kwa maisha ya wengine, na anaweza kufanya uamuzi bora kuhusu maadili ya mwengine, lakini hii si njia ya haki.

Dini ya kiislamu inapinga vikali vitendo vya ushoga na usagaji, na waislamu wengi wanachukizwa na vitendo hivyo.

Previous
Next Post »