Katika makala iliyopita Nilifundisha namna ya kupoa asidi iletayo kiungulia kwenye maharage,na tuliona kwamba huwezi kutoa asidi(phytic)yote kwenye maharage ila unaweza kuipunguza kwa kiasi kikubwa ili kuepusha kiungulia.Kwa mantiki hiyo basi,bado kuna kiasi kidogo cha asidi kinachobaki,kuna watu wachache ambao hata kiasi hicho kidogo cha asidi hutosha kuwapa kiungulia.
Kuna namna ya kukata Asidi kidogo inayobaki kwenye maharage baada ya kuyaloweka,unaeweza ongeza maziwa au nazi.
Ili kuelewa kwanini maziwa na nazi vinakata asidi iliyopo kwenye maharage,nilazima utambue kwamba maziwa na nazi ni BUFFERs(kiingere)buffer ni mchanganyiko wenye asidi na base kwa pamoja. niwarudishe secondary,enzi zile ukiwa kidato cha pili ulijifunza kuhusu acid and base.Naamini mwalimu wako alikwambia base inauwezo wa ku neutrolise acids.Hicho ndicho kinachotokea unapoweka maziwa kwenye maharage,base iliyo kwenye maziwa inakata/ neutrolise ile phytic acid iliyo kwenye maharage.
Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa yakaiva
mafuta ya kula
vitunguu maji
Nyanya
vitunguu swaumu
chumvi
Maziwa
Njia
1.Chemsha maharage adi yaive nay awe laini,hakikisha maji yamekauka kabisa kwenye maharage kabla hujaepua jikoni.Maharage yakiiva na kulainika hupasuka yenyewe
- Usiweke chumvi unapochemsha maharage,chumvi hufanya maharage yawe magumu
- Kawaida mafuta huja juu na nyanya hubaki chini.
4.Ongeza maziwa fresh,kisha koroga ili kuchanganya.weka maziwa yakutosha ili kupata mchuzi wakutosha.maharage hupendeza zaidi yakiwa na mchuzi.Watoto wengi wanapenda mchuzi wa mahage na si maharage yenyewe.
- Unaweza weka maji na maziwa ,katika hili,tanguliza maji yakishachemka ndipo uweke maziwa na uchemshe zaidi.
Maelezo ya ziada
Kama unaamua kutumia nazi,upishi ni kama huu nilioelezea,ila tu pale nilipoatumia maziwa unaweza tumia nazi.
Unapochemsha na kuivisha maharage ,Hakikisha mchuzi au maji yote yamekauka kwenye maharage ,ili kutunza ladha na utamu wa maharage.wengi mnapenda kuacha mchuzi ili muutumie wakati wa kuunga maharage.Unapoongeza mchuzi huo baada ya kuunga,unapunguza nguvu ya maziwa au nazi,na zaidi ya hapo ubaharibu utamu au ladha ya maharage kwani maziwa na nazi huleta ladha nzuri kwenye maharage.
Maharage ni chakula kizuri sana na kitamu,ila kiungulia,gesi tumboni na upishi mbaya unachangia sana watu wengi kutokula maharage,au kutokuyapenda.
Langu mmoja tu,kukufumbua macho,na kama kawaida utendaji ni juu yako.Ipe familia yako maharage bora sio bora maharage.
EmoticonEmoticon