“PRESS RELEASE” TAREHE 12. 06. 2013.
WILAYA YA RUNGWE –
MAUAJI
MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA BUSISYA KATA YA MASOKO WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. CHARLES S/O
SYELUKINO, MIAKA 40,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA BUSISYA ALIUAWA KWA
KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KWA KUTUMIA MAWE NA FIMBO NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA SIMU MOJA YA MKONONI AINA YA NHONG
YENYE THAMANI YA TSHS 50,000/= MALI YA LUMUMBA S/O MWAIPOPO, MIAKA 40, KYUSA,
MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA BUSISYA. MTUHUMIWA MMOJA ZEKIA S/O MWAKYAMI,MIAKA
52,KYUSA,KAIMU AFISA MTENDAJI KIJIJI CHA BUSISYA AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO
ZAIDI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO
WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MOMBA –
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 11.06.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO MTAA WA
MAJENGO TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.SHALZOLE S/O AHMAD, MIAKA 24 2.ABDULAH
S/O AN YASIN, MIAKA 19, 3.MOHAMED
S/O EFEZAL, MIAKA 24 4. ASHA D/O
FQAT RASOOL, MIAKA 22. 5. MOHAMED
S/O ASIM, MIAKA 21 NA 6. ZAHID
BASHIR S/O BASHIR, MIAKA 23 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI PAKISTAN WAKIWA
WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA KIFICHO NA
KUHIFADHIWA NYUMBANI KWA FYUDI S/O SIAME,MIAKA 37,MNYAMWANGA,MKULIMA MKAZI WA
MTAA WA MAJENGO – TUNDUMA AMBAYE PIA AMEKAMATWA .TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA
NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.
WILAYA YA RUNGWE – KUPATIKANA
NA BHANGI
MNAMO TAREHE 11.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA
ENEO LA KIWIRA ROAD TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA MARTIN S/O
KANDONGA,MIAKA 35,MKULIMA,MNDALI MKAZI WA KIWIRA ROAD AKIWA NA BHANGI KILO 5
NYUMBANI KWAKE . MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA
ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 11.06.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA
ENEO LA NJISI- KASUMULU WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA COLINZI S/O MBUGHI,
MIAKA 30,MKULIMA,MNDALI RAIA NA MKAZI WA
MWANGURUKURU – KALONGA NCHINI MALAWI
AKIWA NA BHANGI KILO 3 .MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon