Lipstick ni hatari kwa wanawake wajawazito na watoto

NewsImages/6705586.jpg

Wataalamu wa maswala ya afya ya mama na mototo wamewataka wanawake wenye ujauzito kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya Lipstick, imebainika kipodozi hicho kina material yenye madhara kwa afya ya mtoto.
 
Wataalamu hao wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kupunguza matumizi ya Lipstick, hasa kwa wanawake wajawazito na watoto wa dogo, mmoja ya wataalamu hao akielezea madhara yaliyopo katika kipodozi hicho pendwa kivutio cha wengi amesema, kila lipstick moja ina Material 55% ya madhara kwa afya ya mtoto.

Uchunguzi uliyofanywa na wataalamu hao katika mashirika 22 makubwa duniani yanayojihusisha na utengenezaji wa kipodozi hicho, umebaini kwamba mashirika 12 kati ya 22 yanatumia material yenye madhara kwa watoto, miongoni mwa madhara ya kipodozi hicho, ni kudhofika kwa akili ya motto na kupunguwa uwezo wa kujifunza.

Katika siku za hivi karibuni midomo imekuwa sehemu muhimu sana katika kukamilisha urembo na unadhifu wa wanawake, lipstick imekuwa inawafanya waonekane wana mvuto zaidi na kuongeza kupendeza katika muonekano wao

 
Previous
Next Post »