DINA MARIOS NA WENZAKE 6 WAMECHAGULIWA KUWA MABALOZI WA OXFAM TANZANIA WATAZAME HAPA

 
Ijumaaa ya tarehe 14 june mimi na wenzangu 6 tulisimikwa ubalozi wa Oxfam Tanzania wa kampeni ya GROW.
Kusimikwa huko kuliambatana na tuzo maalum ya kutambulika kwa mchango wetu katika kampeni hiyo.
Muigizaji maarufu Jackob Steven JB
Mbunifu wa mitindo Tanzania Khadija Mwanamboka
CARTOONIST,MTANGAZAJI na mtayarishaji wa vipindi vya tv Masoud Ally wa Kipanya
Blogger maaarufu Shamimu Mwasha
Mabalozi wengine ni mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee na mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mh. Shyrose Bhanji ambao hawakuwepo kutokana na majukumu.
Mkurugenzi wa OXFAM  Tanzania Justin Morgan
TAKWIMU zinaonyesha, tuko watu Billion Saba ulimwenguni hadi sasa.
TAKWIMU hizo hizo zinaonyesha, kati ya hao, takribani watu Billion moja hulala na njaa kila siku hiyo ikiwa ni tafsiri ya takribani mtu MMOJA kati ya watu SABA.
USHAHIDI
upo kwamba chakula kinachozalishwa kinatutosha kula hadi kusaza.
USHAHIDI upo masokoni na sehemu za kuuza chakula jinsi ambavyo chakula hasa mboga mboga na matunda vinavyotupwa baada ya kuharibika.
USHAHIDI upo kwenye mashimo ya taka tunapotupa mabaki ya chakula.
USHAHIDI upo mashambani kwa wakulima wadogo wadogo wanaoacha mazao kuharibikia shambani kwa kukosa soko.USHAHIDI upo kwenye supermarkets chakula kinapotupwa kwa sababu kime-expire..
MAKADIRIO ni kuwa kufikia mwaka 2050 tutakuwa watu BIllion Tisa ulimwenguni.
USHIRIKIANO ni msingi sasa kuhakikisha tunawezesha mfumo wa chakula kuwa wa HAKI na USAWA. Hii ni kuanzia shambani hadi jikoni.
 Balozi mwenzetu mwanamuziki maarufu Afrika Angelique Kidjo
Mchngaji Desmond Tutu
Asilimia 70 ya wakulima na wauzaji wa mazao ni wanawake.
 GROW inataka tuoteshe na kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa Chakula, uimarishaji wa haki na mustakabali wa wanawake wazalishaji wa Chakula na pia kulinda mandhari ya uoto na uhalisia wa sayari yetu.

GROW ni kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na shirika la Oxfam. Kampeni hii inataka tuoteshe na kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula, uimarishaji wa haki na mustakabali wa wanawake wazalishaji wa chakula na pia kulinda mandhari ya uoto na uhalisia wa sayari yetu.
Dunia inazalisha chakula cha kutosha lakini watu wapatao milioni moja wanalala bila kula kila siku. Mbaya zaidi, idadi kubwa ya hao ni wanawake wazalishaji na watoto.
Ni wakati muafaka sasa, kuungana na kutokomeza mfumo huu dhalimu wa chakula.
Namna tutakavyokuwa tunafanya kazi zetu za kibalozi mtafahamu kupitia vyombo mbali mbali vya habari.
Na mie kama balozi ntawahabarisha hapa na katika leo tena.
 
source Dina Marios blog
Previous
Next Post »