“PRESS RELEASE” TAREHE 17. 06. 2013.
WILAYA YA MBARALI - KUPATIKANA
NA BHANGI
MNAMO TAREHE 16.06.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO ENEO LA
IGURUSI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIWAKAMATA 1.JISA S/O ESSAU, MIAKA
18, KYUSA, MKULIMA 2. EDWARD S/O
AMBWENE, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, 3.JULIUS S/O LAZARO, MIAKA 26, MSANGU,
MKULIMA NA 4. CHARLES S/O
JAILOS,MIAKA 28,MKULIMA,MSANGU,MKULIMA
WOTE WAKAZI WA IGURUSI WAKIWA NA
BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 10 .
WATUHUMIWA NI WAVUTAJI WA BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA KYELA - KUPATIKANA
NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 16.06.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA
KYELA-KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA EMANUEL
S/O KISOTOKO,MIAKA 23,MKURYA,MKULIMA,MKAZI WA KYELA-KATI AKIWA NA MISOKOTO SABA
YA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 35 . MBINU NI KUFICHA BHANGI KATIKA MFUKO WA RAMBO.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed By,
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon