·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA
WANANCHI JIJINI MBEYA.
·
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA 01 AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE NDOO YA MAJI.
·
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA
BHANGI WILAYANI KYELA.
·
WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI.
·
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA
BHANGI WILAYANI MOMBA.
·
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA YA KUUZA DAWA ZA BINADAMU BILA KIBALI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA MICHE YA BHANGI.
·
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA POMBE
KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI JIJINI MBEYA.
MNAMO TAREHE 21.02.2014 MAJIRA YA SAA
07:30HRS ASUBUHI MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA
KIUME, MIAKA KATI YA 25-30 ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA
KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA
JADI FIMBO NA MAWE. MAREHEMU ALIKAMATWA WAKATI AKIVUNJA DUKA NA KUIBA VIPODOZI
MBALIMBALI MALI YA DANIEL MWANJALA (40)
DAKTARI, MKAZI WA GHANA JIJINI MBEYA TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA
03:00HRS USIKU HUKO SOKOMATOLA KATA YA MAENDELEO NA TARAFA YA SISIMBA
WILAYA YA MBEYA MJINI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME NA
SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA DHIDI YAO ICHUKULIWE.
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA 01 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE
NDOO YA MAJI.
MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BETH PAKIPO (01) MKAZI WA BUJERA
ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE NDOO ILIYOKUWA NA MAJI WAKATI
AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE WENYE UMRI KATI YA MIAKA 02 – 03. TUKIO HILO
LILITOKEA MNAMO TAREHE 21.02.2013
MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO
KIJIJI NA KATA YA BUJERA TARAFA YA PAKATI WILAYA YA RUNGWE. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA
UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA/KUZIBA MITARO/VISIMA/MASHIMO
YALIYO WAZI KWANI NI HATARI KWA WATOTO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA JITOKEZA.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI WILAYANI KYELA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MACRINE EDSON (32) MKAZI WA IPINDA AKIWA NA KETE 122 ZA BHANGI SAWA NA UZITO
WA GRAM 610. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 20.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI
NA KATA YA IPINDA WILAYA YA KYELA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI, TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA
BHANGI.
WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA
MAJINA YA 1. THABIT SHABAN (28) 2. MICHAEL SIGARA (22) NA 3. JAMES MWANGANDE (22) WOTE WAKAZI WA
MKOMBWE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA
WAKIWA NA BHANGI KETE 14 SAWA NA UZITO
WA GRAM 70. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO
TAREHE 21.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA MKOMBWE KATA YA UBARUKU TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI. WATUHUMIWA NI
WAUZAJI NA WATUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI WILAYANI MOMBA.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA JESI MWAKANGALE (21) MKAZI WA
MTAA WA MWAKA – TUNDUMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA
AKIWA NA KETE 171 ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 855. MTUHUMIWA ALIKAMATWA
KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 21.02.2014 MAJIRA YA SAA
10:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA TUKUYU, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA
WILAYA YA MOMBA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI, TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT
MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI/UKULIMA NA
USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA
ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA
KUFANYA BIASHARA YA KUUZA DAWA ZA BINADAMU BILA KIBALI.
MFANYABIASHARA MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AWAZI
MBALAMWEZI (29) MKAZI WA MSUNGWIJI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA
KUKAMATWA AKIUZA DAWA ZA BINADAMU BILA KIBALI KATIKA KIBANDA CHAKE CHA
BIASHARA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
21.02.2014 MAJIRA YA SAA 16.45HRS
JIONI KATIKA KITONGOJI CHA MSUNGWIJI, KIJIJI CHA ISANGAWANA WILAYA YA
CHUNYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MTUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT
MAYALA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUFANYA BIASHARA BILA KIBALI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA WATUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MICHE YA
BHANGI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA AIDAN MWAKILEMBE (32) MKAZI WA
MSUNGWIJI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA MICHE 111 YA BHANGI YENYE UREFU WA FUTI 05 KATIKA SHAMBA LAKE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 21.02.2014
MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MSUNGWIJI, KIJIJI CHA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MTUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
UUZAJI/UKULIMA NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA LUBHINZA JILASA (44) MKAZI WA
MSUNGWIJI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI YENYE UJAZO WA LITA
AROBAINI [40]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA
MNAMO TAREHE 21.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:45HRS JIONI HUKO KATIKA
KITONGOJI CHA MSUNGWIJI, KIJIJI CHA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MTUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT
MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU
NA SERIKALI.
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 21.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:45HRS JIONI KATIKA KIJIJI CHA
ISONGOLE, KATA YA MATWIGA, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA ILEJE, JESHI LA POLISI
LILIKAMATA POMBE KALI ZILIZOPIGWA
MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA BOSS KATONI SABA [07]. MTUHUMIWA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI NA KUTELEKEZA MZIGO HUO. KAIMU KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT
MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA
KUUZA/KUSAMBAZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA
MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon