Mtangazaji katika super brand redio Clouds Fm juzi alipata tuzo kutoka familia ya Steven Charles Kanumba na alikuwa na haya ya kusema.
Jana April 7 2013 bila kufahamu kitakachotokea nilikwenda viwanja vya Leaders kwa ajili ya kupiga picha na kuchukua habari kwa ajili ya AMPLIFAYA ya Clouds FM na millardayo.com ambapo nilipokua kwenye stage na Camera yangu nikichukua matukio wakati familia ya Marehemu Kanumba ikitoa tuzo mbalimbali kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha Kanumba, ghafla nikiwa sijategemea… nikawa mtangazaji pekee na mwandishi wa website nilieitwa na kupewa hii tuzo ya familia hiyo kutambua mchango wangu, asante sana kwa familia hii, asante kwa watu wangu wote wa nguvu wanaonisupport.
EmoticonEmoticon