MCHEKESHAJI wa kike wa filamu za kibongo, Tumaini Martin ‘Matumaini’ aliyekuwa anaishi Msumbiji, amrerejea nchini jana akiwa hoi.
Matumaini ambaye aliyekuwa amezidiwa kwa ugonjwa huko Msumbiji alipokelewa na wasanii wenzake wa filamu jana mchana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Amana Ilala na kulazwa.
Hali ya msanii huyo si nzuri na mwili wake umedhoohofika sana kwa kile kinachoaminika kuwa ni huduma mbovu za kimatibabu alizokuwa anapata nchini Msumbiji.
Matumaini aliingia Msumbiji katika ziara ya kisanii kisha akampata bwana akaamua kuishi nae kama mke na mume na kufanya maisha yake huko.
EmoticonEmoticon