Ugiriki kupatiwa fedha nyingine leo

 
Mawaziri wa fedha wa kanda inayotumia sarafu ya euro wanakutana leo kwa wiki ya tano mfululizo kujadili suala la msaada kwa Ugiriki, na wanatarajiwa kutoa idhini ya kutolewa kwa fedha hizo zilizosubiriwa kwa muda mrefu.

Waziri wa fedha wa Ufaransa Pierre Moscovici aliwaambia waandishi wa habari wakati wa kikao cha mawaziri wa fedha mjini Brussels jana, kuwa wataamua leo juu ya kutoa fedha hizo kwa Ugiriki.

 Waziri wa fedha wa Ireland Michael Noonan naye alisema anadhani kuwa suala la Ugiriki litapatiwa ufumbuzi asubuhi ya leo. Msaada huo wa euro 34.4 bilioni utaisadia Ugiriki wakati ikiendelea na juhudui za kushughulikia matatizo yake ya kifedha, ikiwemo madeni yanayozidi kuongezeka.
Previous
Next Post »