Hali ya Hugo Chavez yatia mashaka

Makamu wa rais wa Venuzuela na kaimu rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro amewatahadharisha raia wa Venezuela juu ya wakati mgumu unaoikabili nchi hiyo, akisema rais Hugo Chavez anaendelea kupata nafuu lakini kwa matatizo baada ya kufanyiwa upasuaji wa saratani. 

Waziri wa mawasiliano wa Venezuela alisema hali ya rais Chavez ilikuwa imetulia, lakini makamu wa rais alisema upasuaji wake uliodumu kwa saa sita siku ya Jumanne ulikuwa mgumu sana, hii ikimaanisha kuwa hata mchakato wa kupona utakuwa mgumu vilevile.

Chavez aliwambia wavenezuela wakati akierejea nchini Cuba kwa ajili ya upasuaji huo wa pili, kuwa wajiandae kwa lolote lile, na kwamba changamoto hizo wataweza tu kukabiliana nazo kama watakuwa na umoja.

Aina na ukubwa wa saratani ya Chavez na wapi ilipo vimekuwa siri kwa muda wa miezi 18, jambo ambalo limesababisha minong'ono na wasi wasi nchini humo. Chavez alisafiri kwenda Cuba siku ya Jumatatu baada kubainisha kuwa saratani yake imerudi baada ya kuchaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa miaka sita ambao unaanza tarehe 10 Januari.
Previous
Next Post »