Misri kupiga kura ya maoni kwa awamu mbili


Raia wa Misri wanajiandaa kwa ajili ya kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya, ambayo imesababisha mgawanyiko mkubwa nchini humo.

Wapinzani wanahofu katiba hiyo ambayo inaungwa mkono na chama cha rais Muhammad Mursi cha Udugu wa Kiislamu, inaweza kusababisha utekelezaji wa tafsir kali ya sheria za dini ya Kiislamu. 

Lakini maandamano ya wiki kadhaa dhidi ya rais Mursi hayajafanikiwa kumshawishi kubadilisha msimamo wake wa kuendelea na kura ya maoni juu ya katiba hiyo.

Wapinzani wamewataka wafuasi wao wapige kura ya hapana kuikataa katiba hiyo, lakini wametoa masharti ya kushiriki kwao, ambayo yanaweza kuwa magumu kwa waandaaji kuyatekeleza.

Hofu inaendelea kutanda kufuatia vurugu zilizosababisha vifo vya watu wanane na kuwajeruhi wengine zaidi ya 600. Mursi ameamrisha zoezi la kupiga kura ligawanywe katika Jumamosi mbili kwa sababu majaji wengi wamegoma kusimamia zoezi hilo.
Previous
Next Post »