MKUU WA MKOA WA RUKWA AWAPASHA VIONGOZI WA WILAYA YA KALAMBO KUWA KUFANYA KAZI KAMA TIMU NDIO NGUZO YA MAFANIKIO KWA WILAYA YAO MPYA




Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa Wilaya mpya ya Kalambo alipotembelea hivi karibuni kuona jengo ambalo Mkuu wa Wilaya hiyo atalitumia kama ofisi yake ya muda. Aliwataka viongozi pamoja na watumishi kutoweka urasimu mbele katika utendaji kazi na badala yake kuwa kitu kimoja bila kujali cheo cha mtu. "Kila mmoja atekeleze jukumu lake katika eneo lake na kwa kufanya hivyo kutaifanya Wilaya hii nzuri kusonga mbele kwa kasi, kwa watumishi wa kada za chini mnatakiwa kumuona Mkuu wa Wilaya kama rafiki na kumuona muda wowote pale ushauri wake unapohitajika" alisema Injinia Manyanya.
Kushoto na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alipotembelea kuona hali ya ofisi hiyo, Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo machachari ndugu Moshi Mussa Chang'a. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka viongozi hao kuhakikisha suala la mipango miji bora linazingatiwa katika kupanga miji na wilaya kwa ujumla.
Mazungumzo yakiendelea, hata hivo Mkuu huyo wa Mkoa aliwaomba viongozi hao kuwa wavumilivu kwani kutokana na changamoto
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akielezea baadhi ya kero zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Mkuu huyo wa Mkoa aliwapa moyo kuwa watumie uwezo wao mdogo walionao kutatua baadhi ya kero hizo na nyingine watashirikiana kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na viongozi pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Moshi Chang'a.
Jengo ambalo linatumika kwa muda kama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kalambo.
Makazi ya muda ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
 
Previous
Next Post »