Anusurika kubakwa na mjomba wake

NEEMA ATHUMANI [22] alijikuta akitaka kumaliza vibaya mwaka baada ya kunusurika kubakwa na mjomba wake wakati alipokuwa amelala nje ya chumba chao kukwepa joto linalotingisha sasa jijini Dar es Salaam Neema alikumbwa na kadhia hiyo usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kigogo Landabaa usiku wa saa 7 wakati alipokuwa amelala nje ya chumba chao

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, Neema wakiwemo na wadogo zake wawili wa kike walikuwa wamelala nje ya chumba chao katika uwa wa nyumba hiyo kutokana na joto kali linalowakabili hivi sasa wakiwa wanalala usiku katika chumba chao hicho

Imedaiwa familia hiyo yenye jumla ya watu saba akiwemo mjomba wao huyo [binamu wa mama yake] aliyekuja kuwatembelea miezi mitatu nyuma akitokea mkoani Ruvuma

Imedaiwa imekuwa ni desturi yake yeye na wadogo wadogo zake na hata siku nyingine kudaiwa na mama yao huwa wanalala mahali hapo uani kukwepa joto linalowasumbua wakazi wengi wa jiji hivi sasa

Hivyo jana imedaiwa mjomba wake huyo alijikuta akimvizia mpwa wake huyo kwa matamanio ili ambake usiku huo wa saa 7 wakati mabinti hao wakiwa wamejipumnzisha mahali hapo kwa usingizi

Kwa kuwa siku zote Mwenyezi Mungu huwa hamfichi mnafiki kijana huyo [Pasco 27] amejikuta akigonga mwamba katika harakati za kutaka kumbaka binti huyo baada ya Neema kushituka usingizini na kujikuta akiwa haamini kwa kujikuta amesimamiwa na mjomba huyo kisha kumuamuru asipige kelele na kumuomba afanye nae mapenzi kwa siri bila wazazi wake kujua

Mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa mjomba wake huyo imedaiwa Neema alianza kupiga kelele kuashiria haamini masikio yake ndipo mama yake alipotoka alimbainishia na mjomba huyo kutakiwa kuondoka usiku huohuo

Hata hivyo imedaiwa mjomba huyo aliomba kupambazuke na kudaiwa kuondoka majira aya alfajiri kwenda mahali ambapo bado hakujafahamika
Previous
Next Post »