Mama mmoja Mkoani Mara, amechukuwa uwamuzi wa kunywa sumu baada ya kugunduwa watoto wake watatu wamefariki dunia, watoto hao walikufa kwa kukosa hewa, baada ya kuacha jiko la mkaa lililokuwa limeinjikwa maharage likiwa linawaka na kwenda kulala. Mama huyo alichukua uwamuzi huo mgumu na wahatari wa kunywa sumu baada ya kuamka na kugunduwa kuwa watoto wake watatu wamefariki dunia, mama huyo aliwaishwa hospitali na kufanikiwa kutapishwa sumu aliyokunywa.
Watoto hao walikufa kutokana na kukosa hewa katika chumba walichokuwa wamelala ambacho kulikuwa na jiko la mkaa lililokuwa likipika maharage, lna kusababisha
kukosa hewa na kupelekea vifo kwa watoto hao.
Watoto hao watatu waliyofariki ni wanafunzi wa Shule ya
Msingi ya Nyangoto, iliyopo katika Tarafa ya
Ingwe wilayani Tarime Mkoani Mara, Naomi Nyasenso darasa la saba, Magreth Nyasenso darasa la nne na Debora
Nyasenso darasa la kwanza.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime,
Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha, amewashauri wananchi kujenga nyumba na kuweka madirisha makubwa, kwani nyumba hiyo ingekuwa na madirisha
makubwa ya kuingiza hewa, ajali hiyo isingetokea.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon